UTANGULIZI
Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ni miongoni mwa vitengo sita vinavyojitegemea kilichoanzishwa tarehe 08 Juni, 2011.
Kazi kuu za kitengo hiki ni kusimamia mifumo yote ya TEHAMA , kufanya ukarabati na ukarabatikinga kwa vifaa vya TEHAMA kutoa vigezo vya manunuzi na ukaguzi wa vifaa vya manunuzi, kutoa mafunzo ya ndani ya TEHAMA kwa watumishi na kutoa msaada wa kiufundi kwa watumiaji wa TEHAMA
KAZI ZA KITENGO :-
1. Kuhakikisha mifumo ya TEHAMA iliyopo katika Halmashauri inafanya kazi kama inavyotakiwa;
2. Kutoa msaada wa kiufundi kwa watumishi wote wa Halmashauri katika eneo la TEHAMA;
3. Kutoa mafunzo kwa watumishi wa Halmashauri katika masuala ya TEHAMA zikiwemo programmu mbalimbali;
4. Kusimamia sera, mikakati na miongozo inayotolewa na Serikali Kuu juu ya uendeshaji wa mifumo, miundombinu na vifaa vya TEHAMA;
5. Kuibua mahitaji ya mifumo ili iweze kusanifiwa na kisha kutengenezwa6. Kuchambua na kuainisha huduma zinazoweza kutolewa na mifumo ya kielekroniki katika Halmashauri;
7. Kuhakikisha miundombinu kiambo (Local Area Network) katika Halmashauri inafanya kazi na mtandao wa intaneti unapatikana;
8. Kuandaa mpango, bajeti, mpango kazi, mpango mkakati wa kuteleza kazi za TEHAMA katika Halmashauri;
9. Kutengeneza utaratibu mzuri wa kutunza taarifa na data ili ziweze kutumika wakati wa majanga;
10. Kufanya na kusimamia matengenezo ya vifaa vyote vya TEHAMA;
11. Kutafiti na kuchambua matatizo ya vifaa vya TEHAMA na kutoa suluhisho;
12. Kushirikiana kwa karibu na wataalamu wa TEHAMA wa Mkoa na wa Wizara ili kubadilisha uzoefu na kujengeana uwezo;
13. Kutoa specification za vifaa kwa ajili ya manunuzi;
14. Kushiriki katika zabuni za vifaa vya TEHAMA na kuhakiki ubora wake kabla havijaanza kutimika; na
15. Kuhakikisha Halmashauri ina tovuti na inapatikana wakati wote.
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.