Mkuu wa Wilaya ya Mafia Mhe. Aziza Mangosongo ameongoza kikao cha Tathmini ya Mkataba wa Lishe robo ya pili, Oktoba - Desemba 2024/2025 kilichofanyika katika Ofisi yake Februari 05, 2025.
Mhe. Mangosongo amewataka wataalam wa lishe kwa kushirikiana na Idara ya Elimu Sekondari na Msingi kuongeza kasi ya kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa lishe, hasa shuleni kwa kuhakikisha wazazi wanashirikishwa vyema.
Aidha, amezitaka shule zote kuhamasisha masuala ya lishe kwa kuhakikisha wanaandaa na kusimamia vyema klabu za lishe ikiwemo kutilia mkazo uwepo wa bustani za mboga mboga, kwa kupata ushauri mzuri kwa maafisa kilimo.
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.