Mkuu wa Wilaya ya Mafia Mhe. Aziza Mangosongo ameitaka Halmashauri kuharakisha mchakato wa kuhamia Ofisi mpya zilizopo eneo la Chicco ili kurahisisha utoaji huduma kwa wananchi.
Mhe. Mangosongo ameyasema hayo Agosti 28, 2024 wakati wa Mkutano Maalum wa Baraza la Madiwani uliolenga kujadili na kupitia taarifa ya hesabu za Halmashauri.
Akijibu hoja ya Mkuu wa Wilaya, Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Juma Salum ameahidi kuwa mpaka ifikapo Septemba 20, 2024, Halmashauri itakua imehamia kwenye ofisi mpya.
Miongoni mwa mambo mbalimbali aliyoyasisitiza Mhe. Mangosongo wakati wa baraza hilo, ni pamoja na usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo kwa kuanza na uchaguzi mzuri wa maeneo ya utekelezaji wa miradi ili kumaliza miradi kwa wakati. Suala lengine ni usimamizi mzuri wa ukusanyaji wa mapato.
Aidha, amewapongeza viongozi wa Halmashauri pamoja na watumishi kwa kupata Hati safi na kuwataka waongeze juhudi zaidi ili kuchangia maendeleo wilayani Mafia.
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.